Hatua hiyo ilitekelezwa katika hafla maalumu Jumamosi, ikiwa ni baada ya siku arobaini za maombolezo na huzuni zilizotanda katika nyoyo za wapenda Ahlul-Bayt (AS) kufuatia kuuawa shahidi kwa Kiongozi wa Mapinduzi, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, pamoja na mashahidi wengine wa Vita vya Ramadhani.
Katika kipindi hiki cha siku arobaini, mpango mpana wa kupamba maeneo mbalimbali ya haramu na kuyafunika kwa vitambaa vyeusi ulitekelezwa katika sehemu tofauti za malalo hiyo tukufu.
Uwekaji wa maandishi meusi ya kumbukumbu, bendera na vitambaa katika bustani, baraza, na maeneo ya juu ya haramu ulifanya mazingira yote ya malalo hiyo kung’ara kwa sura ya maombolezo yenye utukufu.
Imam Khamenei, akiwa pamoja na maafisa waandamizi wa kijeshi wa Iran, aliuliwa shahidi katika mashambulizi ya kigaidi ya Marekani na utawala wa Kizayuni siku ya kwanza ya Vita vya Ramadhani, Februari 28 sawa na tarehe 10 ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Iran ilijibu mashambulizi hayo kwa kufanya hujuma kadhaa za makombora na ndege zisizo na rubani dhidi ya malengo ya Kizayuni na vituo vya Marekani katika eneo , hatua iliyowalazimu maadui kuomba kusitishwa kwa mapigano mnamo Aprili 8.
3497057